Furahia ulimwengu wa hadithi ukitumia Vitabu vya Google Play! Gundua mamilioni ya vitabu pepe, vitabu vya kusikiliza, vibonzo na manga — vyote katika programu moja.
Vipengele Muhimu:
• Maktaba yako, popote: Furahia vitabu kwenye simu, kishikwambi, kompyuta au hata katika gari lako ukitumia Android Auto. Pia, unaweza kupakua vitabu vya kusoma nje ya mtandao.
• Jipatie pointi za Google Play: Pata zawadi za pointi za Google Play unaponunua vitabu. Kumbuka: Upatikanaji wa pointi za Google Play, viwango vya tuzo na viwango vya kizidishaji hutofautiana kulingana na nchi. Mpango wa pointi za Google Play haupatikani katika nchi zote.
• Panga ukitumia rafu: Weka upendavyo maktaba yako ya kidijitali ukitumia rafu maalum kuainisha vitabu vyako kulingana na aina, mwandishi au mada yoyote ambayo ungependa.
• Kipengele cha madokezo mahiri: Andika madokezo yanayosawazishwa na Hifadhi yako ya Google na yanayoweza kutumwa ili kurahisisha ushirikiano.
• Huhitaji kujisajili: Nunua tu vitabu unavyotaka, unapovitaka.
• Zana za kusoma zinazowafaa watoto: Waruhusu watoto wavinjari ufafanuzi wa maneno na wasikilize vitabu vikisomwa kwa sauti. Kumbuka: Zana za mazoezi ya kusoma zinapatikana katika Kiingereza pekee.
• Vibonzo vya kuvutia: Furahia Kiputo kinachokuza maandishi kwa usomaji maalum wa vibonzo na manga.
• Kagua kwanza kabla ya kununua: Angalia sampuli ili uhakikishe kuwa ni kitabu kinachokufaa.
• Kusoma bila kugusa: Dhibiti kitabu chako cha kusikiliza kwa sauti yako ukitumia programu ya Kiratibu cha Google.
• Soma inavyokufaa: Wekea mapendeleo usomaji wako kwa kurekebisha fonti, ukubwa wa maandishi, mwangaza na zaidi.
Mamilioni ya hadithi yanakusubiri kwenye Vitabu vya Google Play! Pakua sasa kisha uanze kusoma.
Ilisasishwa tarehe
4 Jun 2025