elfu 50+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
PEGI 3
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Zana ya Hesperian Health Guides ya Uzazi wa Mpango hutoa taarifa sahihi na za kisasa juu ya njia za uzuiaji mimba ili watu waweze kuchagua njia inayokidhi zaidi upendeleo na mahitaji yao. Zana hii imebuniwa kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa mstari wa mbele, viongozi wa jamii, na waelimishaji rika. Imesheheni picha, vielelezo na taarifa zinazoeleweka kwa urahisi, na nyezo shirikishi kusaidia majadiliano juu ya afya ya uzazi.

Zana hii, ambayo hupatikana bure na katika lugha tofauti, hufanya kazi bila data na imebeba mada muhimu kwa ajili ya ushauri nasaha juu ya uzazi wa mpango, zikiwemo jinsi kila njia inavyotumika, ufanisi wake katika kuzuia mimba, urahisi wa kuitumia kwa faragha,na maudhi au kero.

NDANI YA ZANA HII:
• Njia za uzuiaji mimba – taarifa juu ya njia za vizuizi, tabia (njia za asili), homoni, na njia za kudumu-kila njia na ufanisi wake, faida na mapungufu yake 
• Nyenzo ya kusaidia kuchagua njia – nyenzo shirikishi ambayo huwasaidia watumiaji kutafuta njia za uzuiaji mimba ambazo zinakidhi zaidi upendeleo wao, mtindo wa maisha, na historia ya afya yao 
• FAQs – sehemu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara inatoa majibu kwa maswali mengi ya jumla juu ya uzuiaji mimba na changamoto za kawaida juu ya njia mahsusi kama vile iwapo unaweza kutumia kondomu moja zaidi ya mara moja, na lini unaweza kuanza kutumia kila njia baada ya kujifungua, mimba kuharibika, au kutoa mimba
• Vidokezo na mifano shirikishi ya ushauri nasaha – boresha stadi zako za ushauri nasaha, kujisikia vizuri katika kujadili taarifa za afya ya uzazi, na kuweza kuwasaidia watu kutoka asili na mazingira mbalimbali 

Baada ya kupakuliwa, zana haihitaji intaneti au data. Lugha za Zana hii: ni KiAfaan, KiOromoo, KiAmharic, Kiingereza, Kihispania, Kifaransa,Kinyarwanda, Kiswahili, Kiganda, na Kireno. Badili kati ya lugha 9 zote wakati wowote.

IMEHAKIKIWA NA WATAALAM. FARAGHA YA TAARIFA BINAFSI.

Kama zilivyo zana zote kutoka Hesperian Health Guides, zana ya Uzazi wa Mpango imefanyiwa majaribio na jamii mbalimbali na kuhakikiwa na watalaam wa afya. Ingawa ilibuniwa kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa mstari wa mbele, inawafaa sana pia watu binafsi wanaotafuta taarifa kwa ajili yao wenyewe au marafiki zao. Zana hii haikusanyi taarifa zozote za binafsi na kamwe taarifa za afya za watumiaji haziwezi kuuzwa au kusambazwa.
Ilisasishwa tarehe
8 Jun 2025

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Hakuna data iliyokusanywa
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha ukusanyaji wa data

Vipengele vipya

Uhuishaji wa maudhui madogo, uboreshaji wa utumiaji.