Imesanifiwa upya kabisa kwa msingi wa mrejesho kutoka kwa watu wengi tangu toleo la kwanza. Ujauzito na Kujifungua Salama sasa ina muonekano na mguso wa kawaida sawa na zana zingine za Hesperian na ipo katika lugha kadhaa. Vipengele vipya muhimu ni pamoja na kikokotoo cha wiki za mimba,vielelezo vilivyoboreshwa, matumizi yaliyorahihishwa na kisaidizi kwa mtumiaji cha ‘Tafuta’ au ‘Search.’ Upana wa maudhui unaruhusu huduma kamilifu juu ya ujauzito,kujifungua na baada ya kujifungua, na unajumuisha mikakati kwa ajili ya jamii kufanya kazi ili kuleta mabadiliko.
Zana imeandaliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa afya na wakunga. Inajumuisha Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiswahili, na Kireno. Hufanya kazi bila mtandao.
Zana ya Ujauzito na Kujifungua Salama hutoa taarifa sahihi na zenye kueleweka kwa urahisi juu ya ujauzito,kujifungua na huduma baada ya kujifungua. Vielelezo na lugha rahisi huifanya zana hii kutumika kwa vitendo na kwa urahisi na wafanyakazi wa afya wa ngazi ya jamii,wakunga, na watu binafsi na familia zao. Zana hii haina gharama, ni nyepesi kupakua, inajumuisha Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na Kireno na hufanya kazi bila mtandao.
Zana imeandaliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa afya na wakunga. Inajumuisha Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, na Kireno. Hufanya kazi bila mtandao.
Zana ya Ujauzito na Kujifungua Salama hutoa taarifa sahihi na zenye kueleweka kwa urahisi juu ya ujauzito,kujifungua na huduma baada ya kujifungua. Vielelezo na lugha rahisi huifanya zana hii kutumika kwa vitendo na kwa urahisi na wafanyakazi wa afya wa ngazi ya jamii,wakunga, na watu binafsi na familia zao. Zana hii haina gharama, ni nyepesi kupakua, inajumuisha Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na Kireno na hufanya kazi bila mtandao.
NDANI YA ZANA
* Kubaki mwenye afya wakati wa ujauzito – jinsi ya kula vizuri, upime nini wakati wa ujauzito, jinsi ya kudhibiti kichefuchefu na matatizo ya kawaida
* kufanya zoezi la kujifungua kuwa salama zaidi – mahitaji ambayo yanapaswa kuwa tayari kabla ya kujifungua, jinsi ya kusaidia katika kila hatua ya uchungu, kutambua dalili za tahadhari na pale huduma ya dharura inapohitajika
* huduma baada ya kujifungua – jinsi ya kumhudumia mtoto na mama mara baada kujifungua, na katika wiki ya kwanza, ikijumuisha kumsaidia kukabiliana na msononeko baada ya kijifungua na katika kunyonyesha
*taarifa za namna ya kutenda – rejea ya haraka ya mbinu za huduma za kiafya kwa kila mada
Kikokotoo cha wiki za mimba
Zana ya Ujauzito na Kujifungua Salama inachangia na kusaidia kazi ya wakunga wauguzi, wakunga wa jadi, waelimishaji wa afya na jamii kuboresha afya ya mama na mtoto duniani kote. Kama zilivyo zana zote kutoka Hesperian Health Guides, imefanyiwa majaribio na jamii na kuhakikiwa na wataalam wa afya. Zana hii haikusanyi taarifa binafsi.
Baada ya kupakuliwa, zana hii haihitaji intaneti. Kama wameunganishwa na inteneti, watumiaji watapata viunganishi kwa taarifa zingine juu ya afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia,na nyenzo kwa ajili ya LGBTQIA+ na watu wenye ulemavu.
Ilisasishwa tarehe
19 Jul 2025